Msanii wa muziki nchini Nigeria, MC Galaxy amejikuta akiambulia lawama nchini Nigeria baada ya kuacha kukatisha video akiwa Live kwenye mtandao wa Instagram huku muigizaji wa filamu na mchekeshaji maarufu nchini humo, Etinosa Idemudia akionesha sehemu zake za siri.
MC Galaxy
Mwanadada huyo alimkuta MC Galaxy akiwa Live kwenye mtandao huo akiongea na mashabiki wake na ndipo alipoanza kumwambia kuwa anataka kumuonesha sehemu zake nyeti.
Etinosa Idemudia ambaye kwenye video alionekana akiwa amelewa huku akiwa na glasi ya bia, alianza kusema “mimi kwa sasa nimechanganywa na mpenzi wangu nimemwambia aondoke chumbani kwangu hataki, sasa nataka MC Galaxy nikuoneshe sehemu zangu za siri kama hataki kutoka chumbani kwangu shauri yake”.
Etinosa Idemudia
Ameeleza mrembo huyo na kuanza kuchojoa nguo zake kuanzia kifuani hadi kwenye sehemu za siri, huku akionesha kwa kamera ya simu.
Wakati akifanya kitendo hicho, alikuwa akilalamika kuwa wanaume wengi wa Nigeria ni wasaliti na hawajui uzuri wa wanawake ndio maana kaamua kuwaonesha mtandaoni.
“Hawa wavulana kila siku wananipa stress, kila siku nakosa furaha wacha nijipe raha mwenyewe. MC Galaxy nakuomba sana usikate video live, kwani kuna watu nataka waone uzuri wangu,“ameeleza mrembo huyo ambaye amekuwa maarufu sana mitandaoni nchini Nigeria.
Hata hivyo, baadhi ya watu wakiwemo wanawake walianza kumshambulia MC Galaxy kwa kumtaka akate video hiyo kwani ni udhalilishaji kwa wanawake.
MC Galaxy baada ya kurekodi video hiyo kwa dakika 18 amesema kuwa alichukulia kawaida na asingeliweza kukata video hiyo na kuwaonya wanawake wengine kuwa tukio hilo likitokea tena hatakata video kwani ni matakwa yao.
Post a Comment