Yule ambae humtaki ndio mumeo
Kwa wadada unaweza kumkataa mwanaume kisa hana hela au ana hela ila roho haijaridhia basi unajiachia kwa vibwana ambavyo vinakuchezea tu mwishowe unatoa mimba unaachwa unasalitia mpaka unazeeka.
Tokea wimbo wa Vaileti mpaka Tetema hujaolewa hujui kwanini kwa maana yule unayemkata ndio kaja kwa wema ila wale unaowapapatikia ndio utaishilia ukitoa macho kama mjusi aliyabanwa na mlango.
Oh mara unasema huyu namchuna mpaka nini .
Mara nina wangu tuna miadi naye ya mbele we have future together mwenyewe hata home hajawahi kuja.
Anawatifuatifua marafiki zako kama nini halafu kutwa masaa ishirini nanne unakuwa unamsema unamuwaza unakuwa unamuota na unajiona kumbe ni mpita njia kazi yake ni kula na kusepa.
Sasa huyo uliyemkataa ataoa utabaki umekomaa hadi ukigongwa na pikipiki sio wewe unajeuriwa na pikipiki umeijeruhi.
Acha kuchagua utajikuta wewe ndio kila mtu anapita akichoka nyumbani kwake. Anajua unachopenda chakula vinywaji na pesa anakuja anakupa anaenda ila hata siku moja hutasikia ndoa.
Utavaa nguo zakila neno hadi ubadili uanze kuvaa vitengee. Utabakia ukiitwa majina kisa ni wewe ulitaka.
Kaa naanaye kupenda tatizo ni hili kumpenda asiyekupenda. Aliyekupenda tulia naye hata hela mkikaa pamoja mkawa serious mtazipata tu.
Au kama anazo basi jaribu kumuweka unavyotaka wewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment