Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema kuwa vikosi vya usalama nchini Venezuela, vikishirikiana na wapiganaji wanaoiunga mkono serikali, vimefanya ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani, kwa kutumia nguvu kupindukia, kufanya mauaji na kuwatesa raia.
Akilihutubia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Bachelet pia ameelezea wasiwasi kuwa vikwazo vya karibuni vya Marekani kwenye biashara za kifedha zinazohusisha mauzo ya mafuta ya Venezuela huenda vikachangia katika kuufanya mgogoro wa kiuchumi kuwa mbaya zaidi.
Ameliambia baraza hilo kuwa serikali ya Venezuela ilishindwa kutambua kiwango cha mzozo wa kiafya na uhaba wa chakula ambavyo vimewafanya Wavenezuela milioni 3 kuhamia nchi za ng'ambo na wakashindwa kuchukua hatua za kutosha kuikabili hali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment