Simba imepangwa kuumana na TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wataanzia nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Dar es Salaam Aprili 4.
Droo ya hatua hiyo ya robo fainali iliyohusisha timu nane, ilichezeshwa jana usiku Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jijini Cairo, Misri.
Timu nyingine zilizoingia katika droo hiyo ni Horoya ya Guinea itakayoumana na Wydad Casablanca ya Morocco, Constantine ya Algeria itakayopepetana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Esperance ya Tunisia na Mamelody Sundown ya Afrika Kusini itakayooneshana umwamba na Al Ahly.
Mshindi kati ya Mazembe na Simba atafuzu nusu fainali na kukutana na mbabe kati ya Constantine na Esperance, wakati mshindi kati ya Mamelod Sundowns na Al Ahly atapambana na mshindi kati ya Wydad Casablanca na Horoya.
Mara ya mwisho Simba na Mazembe zilikutana raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011. Mchezo wa kwanza Wekundu hao walilala mabao 3-1 jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kabla ya kufungwa tena mabao 3-2 nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment