0
Rugemarila Azushiwa Kifo.... Magereza Yakanusha kifo
Jeshi la Magereza nchini limekanusha taarifa za kifo cha mahabusu, James Rugemarila mwenye mashitaka ya uhujumu uchumi, na kusema kwamba yuko salama kabisa.


Akizungumza na www.eatv.tv, Afisa Habari wa Magereza, Lucas Mboje, amesema kwamba taarifa za kifo chake ni za uzushi, na kwamba Rugemarila yuko mzima.

“Msemaji alishakanusha, zilikuwa ni tetesi tu achaneni nazo, mpaka ndugu zake, ni mtu tu aliamua kuzusha kwa sababu zake anazozijua, yeye ni mzima kabisa”, amsema Mboje.

Isome taarifa rasmi iliyotolewa na Jeshi la Magereza hapa chini.

Post a Comment

 
Top