Kikosi cha Simba kinaingia dimbani majira ya jioni leo kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting FC.
Simba inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa imetoka kufuzu na kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga AS Vita ya Congo kwa mabao 2-1.
Kuelekea mechi ya leo Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems, amesema atatumia kikosi mchanganyiko kutokana na wale wengine kuitwa timu za taifa.
Kocha huyo amesema kikosi cha leo kitakuwa mchanganyiko kwa sababu wengine tayari wameshajiunga na timu za taifa kwa ajili kuwania kufuzu fainali za AFCON mwaka huu.
Licha ya nyota wake hao kutokuwepo, Aussems anaamini wanaweza kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting kutokana na upana wa kikosi chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment