HAPATOSHI! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia hivi karibuni kuibuka kwa vita ya maneno kati ya wasanii wawili wa kike Bongo, Irene Charles ‘Lynn’ na Gift Stanford ‘Gigy Money ambapo wamekuwa wakirushiana vijembe na kusababisha kuchafuka kwa hali ya hewa.
Ilidaiwa kuwa, aliyeanza kuchochea moto ni Lynn baada ya kumkejeli Gigy kuwa imekuwaje amekubali kushika mimba na kuzaa, jambo ambalo lilimkera mdada huyo anayedaiwa kuwa mkorofi ile mbaya.
Kufuatia kukejeliwa huko, Gigy juzikati aliibuka na kumchana Lynn kuwa anaongea mambo ya ajabu hasa hilo la kuhoji kwa nini amezaa. “Eti aliniuliza kwa nini nilizaa, swali hilo lilinitoa stimu kabisa. Ilibidi ninunue kwanza bia nyingi ili nizirudishe. Nikajiuliza kwamba ananiambia kwa nini nimezaa kwani yeye ni mwanaume, hazai au ni tasa?
“Mimi simuombei mabaya, mwanaume anayempenda amzalishe yule dada, ile miezi tisa atatoka mdomo wake ameufyata, ataheshimu wanawake wote duniani,” alisema Gigy. Akijibu mashambulizi, Lynn alisema:
“Mimi siwezi kubishana na mtu kama yule, siyo taipu yangu. Inavyoonekana ametumwa sasa nadhani wajingawajinga wametumana.”
Kufuatia bifu hilo lililokuwa gumzo kwenye mitandao, baadhi ya wadau wameeleza kuwa, kuna uwezekano wawili hao wanatumia staili hiyo kutafuta kiki lakini kama ni kweli kuna tofauti kati yao, wakae wayamalize.
“Hili bifu lao nimelifuatilia kwa muda mrefu, huyu anasema hili dhidi ya mwenzake, yule naye anarudisha vijembe. Nadhani inaweza kuwa wanatafuta kiki lakini kama kweli wametofautiana ni bora wakae wayamalize,” alisema Suzan Japhet wa Sinza jijini Dar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment