0
Afariki Dunia Baada ya Kujidunga Sindano ya Matunda
Mwanamke mmoja nchini China almanusura afariki dunia, baada ya kujidunga yeye mwenyewe sindano iliyosheheni mchanganyiko wa matunda yaliyotengenezwa kwa jitihada za kuwa na afya.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51, kufuatia kitendo chake alisababisha idhara kwenye ini, figo, moyo na uharibifu wa mapafu na akawekwa katika uangalizi maalumu kwa muda wa siku tano.

Katika sindano aliyojidunga, kulikuwa na mchnaganyiko wa matunda tofauti tofauti karibu ishirini aliyojidunga kwenye mishipa ya damu,taarifa hii ni kwa muujibu wa mfanyakazi mmoja aliyeko katika Hospitali yenye ushirika na Chuo Kikuu cha Xiangnan kilichoko mjini Hunan alipozungumza na BBC.


Watumiaji wa mitandao nchini China wanadai kwamba tukio la mwanamke huyo limeibua hisia na uhitaji wa ufahamu wa huduma ya kwanza kwa jamii.

Inaarifiwa kuwa baada ya kujidunga mchanganyiko huo wa matunda, mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, akaanza kujihisi ngozi yake inauma na kugeuka kuwa nyekundu, na joto likawa likiongezeka mwilini wake.

Baada ya hali hiyo, alipokwenda hospitalini ikamlazimu kulazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi mnamo tarehe 22 mwezi uliopita, kabla ya kuhamishiwa katika hospitali kuu na baadaye kuruhusiwa.

Tukio hilo limezua mjadala na kugeuka kuwa gumzo nchini China,mitandao ya kijamii ikiwemo mtandao wa kijamii wa Weibo.

Zaidi ya watu elfu kumi na mmoja wa mtandao huo walitumia msemo huu

Mtu mmoja alinukuliwa akisema inaonekana kwamba ''ujuzi wa matibabu wa umma bado ni mdogo sana."

Post a Comment

 
Top