0
Ajiuzulu Urais baada ya kuhudumu kwa miaka 30
Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev ametangaza anajiuzulu baada ya kuwa rais kwa miaka 29.

Nazarbayev ambaye ameliongoza taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta amesema kupitia runinga kuwa amepitisha uamuzi huo mgumu wa kuyafikisha mwisho mamlaka yake kama rais kuanzia kesho.

 Hakutoa sababu maalum ya kujiuzulu kwake. Nazarbayev mwenye umri wa miaka 78, ameliongoza taifa hilo tangu mwaka 1989 wakati nchi hiyo ilipokuwa sehemu ya muungano wa Soviet

Post a Comment

 
Top