0
Rais Museveni ampandisha cheo tena mwanaye Jeshini
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amempandisha cheo mwanaye, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mmoja ya maafisa waandamizi wa Jeshi.

Amepanda kutoka cheo cha Meja Jenerali hadi Luteni Jenerali ambacho ni cheo cha tatu kwa ukubwa kwenye jeshi la nchi hiyo baada ya Jenerali & Field Marshal.

Utakumbuka May 2016 ndipo Rais Museveni alimpandisha cheo mwanaye huyo na kufikia ngazi ya Meja Jenerali ambaye anatambulika kama mtu mwenye nguvu sana katika jeshi la nchi hiyo.

Wengi wanaamini kuwa anatengenezwa kwa ajili ya kumrithi baba yake kitu ambacho wamekuwa wakikipinga vikali.Hata hivyo kwa upande mwingine, Muhoozi amewahi kuweka wazi malengo yake ya kuwa mwanasiasa.

Post a Comment

 
Top