0

Kwanza ni mahusiano ambayo watu au mashabiki wengi hawajayakubali na hili litamfanya Dai ampende zaidi na kuwa prove wrong watu wanao yaponda mahusiano yao.

Lakini watu wanasahau kuwa mapenzi sio ya wengi ni kati ya wawili na wala mapenzi hayaendeshwi na likes za Instagram.

Halafu kingine Tanasha anaonyesha ni mdada mwenye heshima/upendo kwa familia ya mpenzi wake hata kwa mtazamo tuu tusiangalie mavazi yake au kuvuta kwake sigara na ku conclude kwamba ana tabia gani. Kwa wale walioweza kuona ile clip alopost Dai akiwa amempeleka kwao kwa picha ile mnaweza kuona ni binti wa aina gani.

Kingine kinachonifanya nione watadumu yani wameendana na Dai and am sure Tanasha anamuheshimu sana Dai na ndicho wanaume wanataka Heshimaaa uwe umezaliwa ulaya iwe kwenu mabilionea au unahela kumshinda mwanaume, but ukija kwa mwanaume yyte atapenda umheshimu. Ni hayo tuu wadau ngoja tusubiri tuone

Post a Comment

 
Top