GODBLESS Lema Azungumzia Zitto Kufuatiliwa na Wasiojulikana
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema juzi Jumatano Februari 6, 2019 walilazimika kumuondoa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe baada ya kufuatiliwa na watu ambao hakuwataja.
Akizungumza wakati akichangia taarifa ya kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria leo Ijumaa Februari 8, 2019, Lema amesema kama CCM wakitawala kwa haki, kwa kufuata sheria na Katiba hana tatizo hata wakitawala milele.
“Leo mwenyekiti (Mussa Azzan Zungu), Zitto hayuko bungeni tumemuondoa juzi alikuwa anafuatiwa usiku kwa kazi za kibunge sio za kuuza madawa ya kulevya si za kubaka watoto ni kazi za kibunge.”
Lema ameongeza kuwa, “Lengo letu ni kuwaona mnatutawala kwa haki na ndio maana ya upinzani lakini leo hii chuki inajengwa leo kiongozi mmoja M-NEC anasema Lissu akitua ashambuliwe".
Post a Comment