0
Yanga SC yapokea mchango wa laki 7
Klabu ya Yanga imezidi kuneemeka na michango ya mashabiki baada ya kupokea zaidi ya shilingi 700,000 za kitanzania juzi ilipocheza dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Ligi kuu bara Yanga Katika mchezo huo iliibuka kinara kwa ushindi wa mabao 3-1, baadhi ya mashabiki wa Yanga walikuwa wanachangisha fedha ndani ya uwanja.

Mashabiki hao walijitoa kwa hali na mali na kuacha kufuatilia mpira badala yake wakawa wanakusanya fedha na kufanikiwa kufikisha kiasi hicho.

Ikumbukwe si mara ya kwanza kwa wanayanga kuchangisha fedha hizo uwanjani bali imekuwa ni kama jambo la kawaida hivi sasa.

Michango hiyo imekuwa ikishika kasi kutokana na klabu kuyumba kifedha tangu kuachia ngazi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu, Yusuf Manji.

Post a Comment

 
Top