0
Wachezaji watano Simba SC waondolewa katika michuano ya SportPesa Cup
Mbelgiji Patrick Aussems ambaye ni Kocha wa Simba SC, amewaondoa wachezaji wake watano katika michuano ya SportPesa Cup inayoendelea hapa nchini huku jina la nahodha, John Bocco likiwa la kwanza.

Timu ya Simba inatarajiwa kuingia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuchuana na AFC Leopards katika michuano hiyo.

Aussems amesema wachezaji hao amewaondoa kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya majeruhi,
Mbelgiji huyo aliwataja wachezaji hao ni Bocco, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe wote wenye majeraha, Asante Kwasi matatizo ya kifamilia ambaye yupo kwao Ghana na Yusuph Mlipili yeye amemuweka kando kwa sababu ya kiufundi.

“Sheria za SportPesa zinaruhusu kuwatumia wachezaji 22 pekee, hivyo kama kocha tayari nimependekeza wanajeshi wangu nitakaowatumia katika michuano hii.

Hata hivyo amesema wachezaji wake wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji watano pekee ndiyo wanatarajiwa kuikosa michuano hiyo.

Post a Comment

 
Top