0
Pogba kuongeza mkataba Man United, ni baada ya kutimuliwa kwa Jose Mourinho
Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba yupo tayari kuongeza kandarasi ya muda mrefu ndani ya Manchester United itakayomuwezesha kupokea kitita cha pauni 290,000 kwa wiki.


Mfaransa huyo aliyekuwa akilazimisha kutimkia Barcelona dirisha la usajili lililopita kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho sasa yupo tayari kusalia Old Trafford baada ya Mreno huyo kutimuliwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer.

Kwa mujibu wa The Sun, Pogba yupo tayari kusalia United chini Solskjaer huku akihitaji kuboreshwa kwa mkataba wake wa sasa ambao umesalia miaka miwili na nusu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa kwenye kiwango bora zaidi siku za hivi karibuni tangu kutua kwa meneja mpya Solskjaer huku akifanikiwa kufunga mabao matano na kuchangia pasi za mwisho zilizosaidia kupatikana magoli. 

Kufuatia kutimuliwa kwa Mourinho mwezi Desemba, Pogba amejikuta akirudi kwenye kiwango chake ndani ya United.

Post a Comment

 
Top