Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewashukia baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wanaodai kuwa msajili wa vyama vya siasa nchini amepewa madaraka makubwa kupita uwezo wake.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano la kutoa maoni kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa lililoandaliwa na chama cha mapinduzi (CCM), amabpo amekanusha na kusema madai hayo si ya kweli.
Amesema kuwa msajili wa vyama vya siasa si mungu mtu kulingana na mambo aliyopewa kuyasimamia, hivyo amewataka wananchi kujitokeza na kushiriki kutoa maoni yao katika muswada huo na kuachana na propaganda zinazoenezwa mtaani na mitandaoni.
”Kuna watu wanaongea sana kuhusu muswada huu, eti wanasema msajili amekuwa Mungu mtu kulingana na madaraka aliyopewa sio kweli, waacheni na propaganda zao, huu ni muswada mzuri unaotoa dira ya demokrasia nchini,”amesema Polepole
VIDEO:
Post a Comment