Usain Bolt amethibitisha kuwa amestaafu kucheza soka baada ya kushindwa kupata mkataba katika klabu ya Central Coast Mariners ya Australia aliyokuwa akifanya majaribio.
.
''Maisha ya michezo sasa basi, sitaki kusema sikutendewa vyema lakini kwenye maisha tunaishi na tunajifunza pia, kwahiyo nina mambo mengi nitakwenda kuyafanya kwasasa ila kuhusu michezo imetosha'', amesema.
Bolt, ambaye alishinda medali za dhahabu katika mbio za Olimpiki huko Beijing, London na Rio, ameweka wazi kuwa mwelekeo wake wa sasa ni kuendeleza biashara.
Oktoba 12, 2018 Bolt alifunga mabao 2 kwenye mechi yake ya kwanza kucheza ambayo ilikuwa ya kirafiki kati ya Central Coast Mariners na Macarthur South West.
Bingwa huyo mara 8 wa Olimpiki alistaafu mbio mwaka 2017 kwenye mashindano ya Olimpiki ya London, ambapo alipata medali moja ya dhahabu na tatu za shaba huku akishika nafasi ya 3 katika mbio za mita 100.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment