0


Mwanamke anayejulikana Kama Shekha ambaye Wiki iliyopita alitengeneza headlines Baada ya kudai    msanii mkongwe wa Bongo fleva T.I.D sio baba wa Mtoto Wake ingawa amekuwa aking’ang’ania hivo.



Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa Wikienda, kwa njia ya simu akiwa nchini Ujeru­mani, Shekha alisema kuwa anam­shangaa T.I.D anavyokomaa kwamba mtoto ni wa kwake wakati baba halisi ni mwanamuziki wa nchini Kenya, Joseph Makini ‘Prezzo’.

Nimenyamaza kwa muda mrefu lakini sasa nimeshindwa kabisa kuen­delea kuvumilia ndiyo maana naweka wazi na TID ajue kuwa mtoto siyo wake bali ana baba yake.

Uzuri ni kwamba Prezzo ambaye ndiye baba wa mwanangu naye ni mwanamuziki hivyo kama TID anataka amuulize mwenyewe atapata jibu kuhusu nani anastahili kuitwa baba wa mtoto”.

Lakini pia Shekha alimtaka T.I.D kuendelea na maisha yake na yeye aendelee na maisha yake pamoja na mtoto wake kwa sababu hata baba yake ambaye ni Prezzo anamuhitaji pia hivyo waachane kwa usalama hataki malumbano kwani yeye ndiye alisababisha mpaka mambo hayo yakafikia hapo yalipo sasa.

Haya mambo yasingefika huku ila TID ndiye aliyesababisha maana anang’ang’ania vitu ambavyo siyo vyake, naomba aniache jamani na mai­sha yangu huyu mtoto ni wa Prezzo nimemaliza“.

Post a Comment

 
Top