0

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ameibuka na kumwaga povu zito kwa mashabiki ambao wamekuwa wakimuandama na kumponda kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Chuchu na baba Watoto Wake Msanii wa Bongo movie Vicent Kigosi ‘Ray’ wameachana.



Baada ya habari hizo kusambaaa Chuchu aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram iliyomuonyesha akiwa amevaa kibukta kigumu huku kikiacha sehemu kubwa ya mapaja yake na tumbo nje.

Baada ya picha hiyo mashabiki walimsema Chuchu kuwa anafanya hayo kwa sababu ameachna na Ray hivyo anataka kujionyesha huku  wengine wakimtolea maneno machafu.



Chuchu alishindwa kujizua na kumwaga povu zito kwa watu wote ambao walimsema na kuwataka waache kumpangia maisha ya kuishi kwani hawamsaidii kwa lolote wala kwa Chochote.

Post a Comment

 
Top