0

Kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na Kalito Samaki ambaye ni CEO wa Samaki Samaki zote jijini DSM kuhusiana na muonekano wake hasa kuhusu kitambaa anachovaa kwenye jicho lake la upande wa kushoto. Huku wengi wakiwa wamejipa majibu yao na kusema kuwa huenda ni mtindo wake wa tofauti.

Leo January 16,2019 Kalito Samaki ambaye jina lake halisi ni Carlos Bastos ametoa jibu linalomfanya yeye kuvaa patch yaani kuziba jicho lake kwa kifaaa flani hivi kama kitambaa. Kalito pia amepata umaarufu mkubwa kupitia wasanii ambapo ameonekana kwenye music videos mbalimbali

“KILA UBAYA  UNA UZURI WAKE…!!!Mnamo mwaka 2014 nilipata melanoma kwenye jicho langu. Hii ni aina ya kansa , inayotokea mara chache. Kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu
tatizo la kansa sio kwakuwa iko eneo moja itabaki hapo tatizo ni kuwa ina uwezo wa kusambaa mwili mzima na kwa kawaida ikifikia hatua hii una kufa”

“Baada ya kujitambua nikaanza kufanya uchunguzi juu ya saratani na kujaribu kujiuliza ni wapi ilipotokea nikaanza kuutambua ulimwengu mpya taratibu nikaanza kutafuta njia za asili za kutibu saratani, kulingana na chakula na vitu vingine natural kama tahajudi (meditation), yoga, madawa ya mitishamba etc”

“Ile hali ya kuwaza muda wowote utakufa ilibadili sana maisha yangu na kunifanya niwaze tofauti nikaanza kujifunza vitu vipya ni kwa kiasi gani ili kulinda afya yetu tunatakiwa kula vizuri 
Nimejifunza kufurahia kila wakati ninaopata kwakuwa sijui ni lini itakuwa siku yangu ya mwisho maisha yangu yakabadilika na sasa nimekuwa makini zaidi na maisha pamoja na ninayoyafanya”


“Siku zote nimekuwa na mitazamo positive hii ikinifanya kuamini kuwa wakati wangu bado, ninahitaji kuishi.. na hii ikinisaidia sana kuivuka hii hali .Hatimae nimepoteza jicho langu ila nikafanikiwa kuyaokoa maisha yangu mimi ni mzima baada ya kupigana karibua mwaka mmoja na kansa”

“Ulikuwa wakati mbaya na mgumu lakini pia ulikuwa wakati mzuri kwenye maisha yangu kwakuwa kila kitu kilibadilika na kuwa kizuri zaidi… nikawa mtu mpya, nikatambua umuhimu wa familia nikatambua ni kwa kiasi gani napaswa nishukuru kwa maisha niliyonayo sasa nina elimu kubwa kuhusu afya pia ambayo itanizaidia maisha yangu yote”

“Naamini kila jambo baya lina uwezo wakugeuka na kuwa jambo zuri kama ukiamini naamimi huu ulikuwa mtihani kunifanya niwe jasiri na pia kunifundisha somo nahisi labda alikuwa malaika alietaka nijifunze ili nisife”

“Navaa patch kwakuwa nahisi nina muonekano mzuri zaidi nikiwa nimevaa kuliko nikitoa pia ni utambulisho wangu,my style nahisi malaika walitaka mimi niwe na muonekano huu mpya hivyo wakachukua jicho langu 😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣#MisheZangu”

VIDEO:

Post a Comment

 
Top