0
Baada ya Kunusurika Kifungo Huu ndo Ujumbe Aliouandika Chriss Brown
Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Christopher Maurice Brown alimaarufu Chris Brown ametoa ya moyoni baada ya kuachiliwa na Polisi wa mjini Paris nchini Ufaransa kwa tuhuma za ubakaji, huku ikidaiwa ameachiliwa bila kufunguliwa shitaka lolote linalohusu tuhuma hizo.


Ikumbukwe msanii huyo alikamatwa jana mjini Paris kwa tuhuma hizo ambazo mwadada mmoja alifungua mashtaka hayo akidai kuwa Chris alimbaka.


Kwa mujibu wa US. News, Tukio hilo limetajwa kufanyika January 15 – 16 mwaka huu baada ya kikao kwenye kumbi moja ya usiku nchini Ufaransa. Mwanamke huyo (24) alifungua shauri hilo kwa maelezo kuwa Breezy alimualika kwenye chumba cha hoteli ya Le Mandarin Oriental ambapo aliishia kumbaka, ambapo hata mlinzi wake alikamatwa kutokana na tuhuma hizo.


Sasa baada ya tukio hilo kutokea Chris ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram..

I WANNA MAKE IT PERFECTLY CLEAR…… THIS IS FALSE AND A WHOLE LOT OF CAP! NNNNNNNNEEEEEEEEEEVVVVVVVVVVEEEEEERRRRRR!!!!!! FOR MY DAUGHTER AND MY FAMILY THIS IS SO DISPRESPECTFUL AND IS AGAINST MY CHARACTER AND MORALS!!!!!

Akimaanisha ” Nataka kuweka hii habari kwa uwazi kidogo, Huu ni uongo kabisa, kwa binti wangu na familia yangi ni utovu wa nidhamu kabisa na kwa hadhi yangu”


Post a Comment

 
Top