Baada ya Kumhoji CAG, Hii Ndio Kauli ya Kamati ya Bunge
DODOMA: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka, amesema kamati yake imemaliza kumhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad.
Akizungumza na wanahabari baada ya mahojiano ya Kamati hiyo, Mwakasaka amesema; “CAG Prof. Assad amefika leo mbele ya kamati baada ya wito aliopewa na Spika na tumemhoji. Sisi kwa kanuni zetu hapa tunamwita mtuhumiwa, tukishakamilisha hili suala tunalipeleka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai,” amesema Mwakasaka.
Aidha, Mwakasaka amesema Prof. Assad ameonyesha ushirikiano mkubwa kwa maswali aliyoulizwa kamati hiyo.
Januari 7, 2019 Spika Job Ndugai alimtaka CAG kufika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli yake ya aliyoisema akiwa nje ya nchi kwa kusema kuwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dhaifu.
Post a Comment