0
UVCCM Yafunguka Sababu za Utenguzi wa Jokate

Baada ya Jokate Mwengelo Kutenguliwa nafasi yake jana Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka ametaja sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa umoja huo, Jokate Mwegelo.

 Shaka alisema uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Utekelezaji ya umoja huo chini ya mwenyekiti wake, Kheri James kupitia kikao cha siku moja kilichofanyika mjini Dodoma.

Alisema mwanasiasa huyo kijana ameondolewa kwa kuwa nafasi hiyo alikuwa akikaimu kwa takribani mwaka mmoja.

“Alikuwa anakaimu na hakuwa amethibitishwa kuwa mkuu wa idara kwa kipindi chote cha mwaka mmoja. Mara nyingi ukikaimu ni sawa na kusema upo kwenye majaribio.

“Sasa waliokuwa na mamlaka, ndiyo wanaoweza kuamua kwamba sasa iwe hivi au iwe vile. Alikaimishwa na kamati ya utendaji, kamati hiyo hiyo imeamua kutengua uteuzi wake,” alisema Shaka.

Kuhusu madai kwamba Jokate ameshindwa kuimudu nafasi hiyo, Shaka alisema, “Ukikaumu unakuwa hujathibitishwa pengine hao waliokupa nafasi wanakuwa wametathmini vitu vingi sana.”

Jokate aliteuliwa Aprili mwaka jana kukaimu nafasi hiyo.

Post a Comment

 
Top