0

Utafiti mpya ambao umefanywa siku za hivi karibuni na kampuni ya Kijerumani inayojulikana kama Bertelsmann Foundation, ambao umeangalia mataifa 129 duniani umebaini kuwa demokrasia inazidi kushuka kwenye mataifa mbalimbali duniani.

Inaelezwa kuwa ubora wa demokrasia na mifumo ya uchumi wa masoko katika nchi zinazoendelea unaendelea kushuka kwa kiwango cha chini zaidi katika miaka 12 iliyopita, hii ni kwa mujibu wa utafiti huo ambao wameupa jina Mpango wa Mabadiliko (Transformation Index 2018).

Ripoti hiyo imeangalia katika nchi hizo 129 maeneo kama demokrasia, uchumi, utawala. Watafiti hao wameonya kuwa demokrasia iko “chini ya shinikizo” huku ukandamizaji na unyanyasaji wa kisiasa ukiongezeka.

Post a Comment

 
Top