Msaga Sumu ameeleza hayo katika kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kusikia kauli ya Fid Q ilikuwa inadai utunzi wa nyimbo za singeli umekaa kihuni na usela mwingi jambo ambalo kwa mtazamo wake anahisi anarudishwa nyuma katika ile miaka ya muziki kuonekana hauna maana ni uhuni mtupu kwa jamii.
"Ungekuwa muziki wa kihuni inamaana hata serikali ingeingilia kati suala hilo, chamsingi mtu anatakiwa akaushe tu kuongelea mambo mengine. Haya ni maisha na huu ni muziki kama anavyoona mingine tena muziki huu unaweza kuwa bora kuliko ambao wao wanaofanya. Singeli inapendwa na kila rika", amesema Msaga Sumu.
Pamoja na hayo, Msaga Sumu ameendelea kwa kusema "yeye kama hana mambo ya kufanya akaushe kama mwenzake Afande sele. Fid Q ndio mtu wa kwanza namsikia kusema muziki huu ni wakihuni tokea nazaliwa huu ni wivu na roho mbaya kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyewahi kuzungumzia hii roho mbaya lakini labda nimwambie tu amechelewa".
Mtazame hapa chini Msaga Sumu na Fid Q wakifunguka mengine zaidi.
Post a Comment