Baadhi ya Mapedeshee wa enzi hizo Wakiwa na Warembo Katika kipindi cha Mboni Show |
Kwa wale mashabiki wa mziki wa dance nchini,hasa bend za Fm Acadamia,Twanga pepeta,Malaika Bend,Acudo impact,Mashujaa band,Msondo Ngoma,Sikinde n.k mtakua mashahidi katika hili,
Miaka michache iliyopita nyuma kulikua na wimbi kubwa la vibopa,matajiri au kwa jina lingine mapedeshee wa jiji hili la Dsm waliokua wakiimbwa sana na kutajwa tajwa kwenye nyimbo za bendi hizi kila mara au kwenye matamasha ya bendi hizi,hii ilipelekea wao kutawanya au kugawa pesa nyingi kwa wanamuziki husika (hasa wenye asili ya Congo) na kwa mashabiki pia hasa dada zetu wa bongo movie na wasanii.
Wakati mwingine walikua hata wakigawa dola ya mmarekani na euros.
Jambo la kushangaza siku hizi siwasikii wala kuwaona wakifanya kufuru hizo,
Napatwa na mashaka pengine nini kimewakuta?au wameamua kwenda kutapanya nchi za jirani kama Malawi na Msubiji?
Wadau unaweza mtaja pedeshee uliyekua unamwamini sana kwa kutapanya au moja ya tukio uliloshuhudia akitapanta.
Binafsi nakumbuka kufuru ya Pedeshee Ndama mutoto ya ngombe na Pedeshee Bitus dhahabu...wadau wakubwa wa Fm Academia wazee wa Ngwasuma popote pale ndani ya jiji hili hasa Mango Gardern na maeneo mengine.
By Jembelamkono
Post a Comment