Akizungumza na wanahabari leo, jijini Dar, Fatma Karume amesema kuwa baadhi ya viongozi waliwahi kusikika wakijinadi kushinda uchaguzi hata kwa kile walichoita magoli ya mkono na kudai kuwa haki ya kura sasa inaonekana haina thamani, hivyo wao wanataka kuipigania haki hiyo.
Aidha, Fatma Karume amesema watu ambao waliweka mfumo huo wa wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi walikuwa na lengo lao na walifanya hivyo kwa kuwa walikuwa wanajua nini wanataka kufanya.
“Mtu akipiga kura haina thamani yoyote na matakwa yake hayasikilizwi kwa sababu kuna kitu kinaitwa goli la mkono, linalotoka kwenye mfumo ambao refa anaona. Refa wa haki hawezi kukubali goli la mkono. Nini kinafanya refa afumbe macho, asione watu wanaosema watashinda kwa goli la mkono. Kila mtu ana haki ya kupiga kura na ikahesabika. Kama kuna watu wanapiga magoli ya mkono haki yako hii inachukuliwa, yaani imetekwa.Pia alisema kwa mujibu wa katiba ya nchi, msimamizi wa uchaguzi harushusiwi kuwa chini ya chama chochote cha siasa huku akidai wasimamizi wa kura wanavaa magwanda ya chama siku moja siku ya pili wanavaa sare za Tume ya Uchaguzi.
Baada ya kubainisha mapungufu hayo ya sheria, Fatma Karume akasema watakwenda mahakamani kuhoji kama mfumo huo unakubalika chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inataka kila kura ihesabike na demokrasia ifuatwe.
Post a Comment