Vanessa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na Bill Sepenga kuhusiana na mauzo ya albamu kama yanaenda vizuri au laa.
"Mauzo yanaenda sana kusema ukweli yani nimestaajabishwa sana na mauzo ya albamu, nimefurahi kuona watu wapo teyari kupokea albamu. 'Is fun' kuona watu wengine wanataka kunivunja moyo. Mimi naenda baa nauza 'CD' mwenyewe wengine wananifukuza wananiambia albamu zimepitwa na wakati", amesema Vannessa.
Kwa upande mwingine, Vmoney amesema anawashukuru watu wote wanaondelea kumpa ushirikiano kwa namna moja ama nyingine katika kununua albamu yake ya kwanza kwa mwaka 2018.
Post a Comment