0
Msanii wa muziki Bongo kutoka label ya WCB, Rayvanny amesema Jason Derulo muda wowote ataposti ngoma ‘Tip Toe Remix’ waliofanya pamoja.

Hata hivyo muimbaji huyo amesema kuwa hata asipofanya hivyo kitendo cha kukubali kufanya naye kazi ni heshima kubwa amempatia.

“Atapost, kwa sababu ujue unavyoendesha page zako kuna ratiba unakuwa umepanga, so kuna vitu ambavyo nimeshaongea naye najua ni muda gani ataposti,” amesema Rayvanny.

Tip Toe ni ngoma ya Jason Derulo ambayo amemshirikisha French Montana, ngoma hii ilitoka December 7, 2017. Rayvanny ameshirikishwa katika remix ya ngoma hiyo

Post a Comment

 
Top