Mwanamuziki wa Bongo Flava, Feza Kessy amefunguka sababu ya kuandika ngoma yake iitwayo Kaa Kijanja ambayo amemshirikisha Nikki wa Pili.
Muimbaji huyo ambaye ni mtangazaji pia wa Choice Fm, amesema katika maisha yake ilitokea akampenda mtu ambaye hakuwa na muda naye.
“Napenda kulazimisha vitu vitokee lakini kwenye mapenzi hapana, kwa sababu kuna mtu nilikuwa nalazimisha mapenzi lakini hakuwa upande wangu,” amesema Faza.
Ameongeza kuwa kitu hicho kilimkatisha tamaa kwani licha ya hivyo aliyempenda alikuwa akimsaliti katika mapenzi, hivyo akaamua kuondoka katika mahusiano hayo.
Fezza Kessy kwa sasa anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Simple ambayo amemshirikisha Dammy Krane, mdundo ukiwa ni wa producer S2kizzy.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment