Katika historia ya Kanisa Katoliki duniani ni mwiko kwa Padri kuoa, lakini hii iko tofauti kwa Fr. Patrick Henry Edet, ambaye yeye ametangaza kufunga ndoa baada ya mwili wake kuzidiwa nguvu ya nafsi.
Padri huyo ambaye mwaka jana mwezi Novemba alitengwa kwa muda na kanisa la Roma katika jimbo kuu Katoliki la UYO nchini Nigeria, amesema kuwa kwa sasa haoni umuhimu wa kuendelea kuiumiza nafsi yake kwa kile anachoamini kuwa kuoa sio dhambi bali ni utamaduni tu wa kikatoliki ambao hauna maana kwa sasa.
Fr. Henry ambaye amehudumu kwa miaka 11, amedai kuwa huu ni muda mwafaka kwa Wakatoliki kufikiria suala hilo kwani kuna matatizo mengi yanatokea kwenye taasisi hiyo, ambayo yanatokana na sheria ya kutokuoa au kuolewa kwa watumishi.
“Kuanzia leo, naachana na masharti magumu ya Kanisa la Kikatoliki, mwili wangu umeshindwa na nguvu ya nafsi. Mtanisamehe wale wote waumini ambao nimewaudhi kwa maamuzi yangu, mimi ataka niishi kwa ajili ya Mungu hivyo ni lazima nitimize andiko lake la kuzaliana duniani. Ninataka kuwa mtu huru wa mwili na nafsi na kwa andiko hilo natangaza rasmi kuwa mwezi Machi 17 mwaka huu nafunga ndoa hivyo basi nitakuwa muumini wa kawaida,“amenukuliwa Fr. Henry na gazeti la NewsDesk la Nigeria .
Kanisa Katoliki nchini Nigeria limekuwa likikubwa na kashfa mbalimbali za kinidhamu baina ya viongozi wa dhehebu hilo nchini humo, mwaka jana Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis aliwataka mapadri wote nchini humo kumuunga mkono Askofu Mkuu wa Jimbo la Ahiara aliyemsimika baada ya tamko la mapadri nchini humo kukataa usimikwaji wake.
Mwaka 2015 wakati Kiongozi huyo mkubwa wa Kanisa Katoliki duniani alipozuru nchini Kenya, Kanisa Katoliki Nigeria walimtaka aiangazie nchi hiyo ikiwemo kufikiria namna ya kuboresha baadhi ya masharti magumu ya viongozi wa dhahebu hilo ikiwemo ya kuoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment