Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kimeongea na waandishi wa habari leo katika Makao makuu yao
Mbowe amesema Usalama wa Taifa wanaratibu mikakati ya kuwabambikizia kesi wana CHADEMA na wao wamejipanga kutokana na huo mkakati. Amemwambia Rais Magufuli kuwa wapo tayari kwa lolote maana wanapigania demokrasia
Mbowe amesema Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuwabambikizia kesi viongozi wao. Lakini hata kwa mauaji, Mkoa huo unaongoza maana kuna historia ya watu wa CHADEMA kuuawa.
Amemuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Amosi Makala kwenye kuratibu kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu).Amesema hukumu ilifahamika na ilipangwa Hotelini, wote walifahamu na Amosi Makala anajua hilo
Aliongeza kwa kusema “CCM kama wanataka kurudisha uhalali wao wa uongozi waseme na wananchi watawaelewa na sio kutumia bunduki kukatisha uhai wa watu. Halafu tumeshaanza kuzoea kuuwawa, hili jambo si zuri maana tunakoelekea ni kutaka kuua upinzani”
Post a Comment