0
Tangu Nimtongoze Zari, Hadi Sasa Sijawahi Kutongoza Msichana Mwingine- Diamond
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa tangu amtongoze mzazi mwenzie, Zari mwaka 2014 ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kufanya hivyo hajawahi tena kutongoza mwanamke mwingine.

Diamond Platnumz amesema kuwa hawajahi kutongoza mwanamke mwingine kwa sababu yupo na Zari tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya kuwa maarufu.

Akijibu swali kwenye mahojiano yake na Kituo cha Radio cha Kiss FM cha nchini Rwanda, swali lililohoji kuwa alishawahi kukataliwa na mwanamke kabla ya umaarufu wake? Diamond alijibu kwa kusema ‘ndio tena wengi tu kwanini isitokee“.

Na alipoulizwa ni lini mara yake ya mwisho kukataliwa na mwanamke au kusikia neno hapana kutoka kwa mwanamke Diamond Platnumz amesema “tangu nimtongoze Zari, hadi sasa sijawahi kutongoza msichana mwingine“.

Diamond Platnumz wikiendi iliyopita alikuwa nchini Rwanda ambapo akiwa huko alitembelea kituo cha Jordan Foundation kinacholea watoto wenye ulemavu wa macho (Vipofu).

Post a Comment

 
Top