0
"Bob Junior Anaogopa Kusema Ukweli" - Amber Lulu
Msanii Amber Lulu hapo jana alikanwa kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Bob Junior, amefunguka na kudai kuwa msanii huyo anaogopa kusema ukweli.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Amber Lulu amesema tukio hilo lilitokea siku nyingi akiwa mdogo, hivyo huenda Bob Junior anaogopa kukiri kwa kuwa lilikuwa kosa kisheria.

"Sasa kwa nini nimsingizie, labda anaogopa lakini ilikuwa siku nyingi na nilikuwa mdogo, sina sababu ya kumsingizia kweli nilikuwa naye, labda uoga wake, nimsingizie mimi na yeye nani ana kiki!", amesema AMber Lulu.

Hapo jana Bob Junoir alikana kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii AMber Lulu akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili, baada ya Amber Lulu kutoa siri hito huku akisema ndiye aliyemleta Dar es salaam.

Post a Comment

 
Top