0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salamu pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi kilichotokea usiku wa kuamkia leo mjini Dubai, Falme za Kiarabu. Chini ni taarifa ya kiongozi huyo.

Nimepokea kwa majonzi makubwa sana kifo cha Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi, natuma salamu za pole kwa Watanzania na Wana- Afria Mashariki wote, hususani tasnia ya habari, michezo, wafanyabiashara, wafanyakazi wa Kampuni ya IPP, ndugu jamaa na marafiki.

Hakika Taifa limepoteza mtu muhimu sana, aliyejitoa kusaidia Watanzania wenzake katika mambo mengine. Ni kipindi kigumu kuliko wakati mwingine wowote katika maisha ya mwanadamu.

Reginald Abraham Mengi, hakika Taifa litakukumbuka ukiwa mmoja wa watu walioleta mapinduzi katika sekta ya habari na mambo mengine mengi ambayo yatafanya usiweze kusahaulika.

Kimwili haupo nasi lakini hakika matendo yako yataishi kwenye mioyo ya Watanzania. Wewe umekuwa mfano wa kuigwa, hakika tutakukumbuka.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.Upumzike kwa amani Dkt Reginald Abraham Mengi. We will mourn, until we join you Hero. Mwisho.

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi amefariki dunia, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari alivyokuwa anavimiliki. Mengi ambaye ni mmoja kati ya wafanyabishara wakubwa Tanzania amefariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi akiwa Dubai.

Post a Comment

 
Top