Mwanamke mmoja aliyefungua kesi ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya RKelly ameshinda kesi baada ya nguli huyo wa R&B kushindwa kufika mahakamani.
.
Mwanamke huyo ambaye anadai kuwa Kelly alikuwa akimfanyia vitendo vya unyanyasaji wakati ana umri wa miaka 16 alifungua mashtaka siku moja kabla #RKelly hajakamatwa kwa kesi za unyanyasaji wa kingono mwezi februari.
.
Kesi itasikilizwa tena mwezi ujao ambapo jaji ataamua kiasi ambacho @Rkelly atatakiwa kulipa. Rkelly hata hivyo hajawahi kukubali shtaka lolote la unyanyasaji wa kingono japo hata sasa anakabiliwa na kesi nyingine 10 tofauti za masuala hayo hayo ya unyanyasaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Post a Comment