BAADA ya droo ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya kupangwa leo na Barcelona kupangiwa kucheza na Manchester United ikianzia nyumbani, shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), limefanya mabadiliko.
Mechi ya kwanza ya Barcelona na Man United ilipangwa kuchezwa Camp Nou, lakini UEFA wameibadilisha na sasa itachezwa Old Trafford na mechi ya marudiano itachezwa Camp Nou.
Mabadiliko hayo yamakuja kwa sababu, Man City pia mechi yao ya pili watacheza nyumbani, hivyo timu hizo haziwezi kucheza mechi za nyumbani katika usiku mmoja, au unaofuatana.
Maamuzi hayo yamefanywa muda mfupi tu baada ya droo na mamlaka ya ndani ikitajwa kuwa ni sababu za kiusalama.
Man United wamekuwa wahanga wa kubadilishiwa mechi hii kutokana wao walimaliza chini ya Man City katika ligi kuu msimu uliopita lakini kama wangemaliza juu Man City ndio wangebadilishiwa mechi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment