0

Habari wakuu,

Spika anasema Nassari hana sifa ya kuendelea kuwa Mbunge, Hajahudhuria mikutano waka kikao chochote kwa miezi tisa mfululizo.

Spika anasema "Labda nifafanue kwa Watanzania, kuna neno Kikao na neno mkutano. Mkutano ni ule mmoja ambao unakuwa na urefu wake mzima. Kama huu ambao tunauanza na tumeshaanza kamati zake, huu ni mkutano wa 15. Yaani kwa Mwaka mmoja tuna mikutano minne. Kila mkutano mmoja katika hiyo minne ukifanyika kwa siku 10 basi kuna Vikao 10, ukifanyika kwa siku 40 basi huo mkutano utakuwa na vikao 40. Ndo tofauti ya Mkutano na Vikao.

Kwahiyo yeye Mheshimiwa Nassari hakuhudhuria Mikutano Mitatu. Kwa Mwaka tuna Mikutano minne, kwahiyo ndo kusema kwamba Nassari hajahudhuria Kamati au Bunge lenyewe kwa miezi tisa mfululizo. Kwakweli katika Maisha ya kawaida, mtu uliyepewa jukumu la kufanya tena umepewa na wananchi, umeaminiwa na wananchi halafu wewe kwa miezi 9 mfululizo huhudhurii kikao chochote cha kamati wala cha bunge lenyewe, Halafu ukiulizwa unasema ulikuwa unauguliwa, kwakweli kidogo sidharau kuuguliwa. Taratibu zinasema kama una jambo la dharura toa taarifa kwa Spika, Sikuwa na taarifa yoyote inayohusu zuio la yeye kutokuhudhuria bunge kwa miezi tisa, ni muda mrefu sana hata kama kuna tatizo bunge lingejua'" Amesema Spika Ndugai.


Spika akaendelea kusema, "Nimeona barua ambayo hata haijasainiwa, na hata kwenye mafaili yetu barua hiyo haipo na huo sio utaratibu. Hakikisha Spika anapata taarifa, maana yake mpe barua kwa dispatch Spika mwenyewe, wao wapo kwenye chama cha siasa na chama chake ni chadema, na wana kiongozi, kiongozi wake angenipa taarifa ya mwenyewe, naibu kiongozi angenipa. Hakuna aliyenipa taarifa yoyote kwa miezi tisa. Kwahiyo hajaonewa na mtu yoyote hayo ni maneno ya Mkosaji.

Ni kweli wakati nampa hizi taarifa alikuwa kwenye kamati ya bunge anafanya kazi kule Moshi. "Hiyo ni kweli. lakini hiyo haihesabiki katika vile vikao vyangu ambavyo kikatiba vinamtaka. Hiki ndio kikao cha nne cha Mwaka. Katiba inasema ukikosa mikutano Mitatu, yeye alishakosa mitatu, hata kama huu ningemruhusu ahudhurie mpaka mwisho, bado angekuwa hana sifa kwa vile mikutano mitatu kwa miezi tisa hajahudhuria bunge wala kamati yake wala kureport chochote kwa Spika, wala hana barua ya Spika ya kukiri kupokea barua au chochote kutoka kwake. Wala hana barua ya Spika ya ruhusa ya hilo jambo alokuwa akiliombea." Kafafanua Spika Ndugai.

Post a Comment

 
Top