0
Nassari Ashindwa Kuzungumza na Wanahabari Juu ya Kuvuliwa Ubunge
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Kaskazini imesema Mbunge wake Joshua Nassari amekwama kuzungumza na waandishi wa habari juu ya kueleza kilichotokea mpaka akavuliwa Ubunge, na kusema amepanga kuzungumza kesho.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Moses Joseph, amesema Mbunge Nassari alipanga kuzungumza leo, Machi 16, 2019, lakini kutokana na sababu zilizopo neje ya uwezo wake ameamua kusitisha kuzungumza suala hilo akiwa Arusha na atakuja kulizungumza Dar es salaam .

"Kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo imebidi afanye mkutano wake kesho na waandishi wa habari, pale ofisi za makao makuu Dar es salaam", amesema Moses.

"Kuhusu kuficha kitu hakuna kwa sababu (Nassari) alikuwa Arusha kwa hiyo mwanzoni tulijua atafanya Arusha lakini imembidi akafanyie makao makuu." ameongeza Moses

Mapema wiki hii Spika wa Bunge Job Ndugai, alitangaza kumvua Nassari ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa makosa ya mahudhurio hafifu bungeni ikiwemo kukosa vikao vya mikutano mitatu ya bunge


Post a Comment

 
Top