0
Nassari Aanza Safari ya Kupigania Ubunge Wake
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari ameanza safari ya kupigania ubunge wake ambao alivuliwa na Spika wa Bunge wa Job Ndugai kwa makosa ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoituma Joshua Nassari amesema Marchi 18, 2019 ndiyo alifungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga hatua hiyo ya Spika ya kumvua ubunge.

Aidha taarifa yake imesema kuwa kesi hiyo imesogezwa mbele hadi Machi 26, kwa ajili ya upande wa Mwanasheria Mkuu kupeleka majibu ya madai ya msingi ya washtaki na Machi 27 kesi hiyo itaanza kusikilizwa.

Aidha Mbunge huyo ameeleza wameomba kuwekwa kwa zuio la Mahakama kwamba kusifanyike uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo hadi pale kesi ya msingi itakapokamilika.



Post a Comment

 
Top