0
Ameandika RickNess/JF

Nianze kwa kusema kua,nimekua nikimfuatilia sana na kwa ukaribu Joshua Nasari,akiwa bungeni na Jimboni. Joshua anajua kujenga hoja,anajua kuipangilia hoja yake na akaeleweka na wenye akili. Kwale wakuunga mkono kila kitu huwa inakua ngumu kidogo kumuelewa Nasari.

Jimboni kwake nimepita mara nyingi,huwezi kumsema vibaya ukaeleweka. Anasifika kwa uchapakazi wake,na kuhudumia wananchi wake,na alikua kiongozi anayeongoza na kufuatwa na anaowaongoza siyo kwakua walimuogopa,hapa,kwakua tu walimkubali na kumuamini.

Nasari alikosea hapa,

1.kulewa sifa,akadhani tupo kwenye zama zile.

2.kujisahau,na hili ni tatizo la wabunge karibu wote,wanakujaga kugutuka yakiwakuta kama hili la Nasari au kuanza kukataliwa majimboni kabla hata ya uchaguzi.
Mfano mzuri ni mkuu mmoja wa mkoa sasahivi,alienda msibani mwaka 2015,alikua hajawahi kufika eneo hilo tangu uchaguzi wa 2010,alichoambiwa na wafiwa ni"ondoka tuzike,maiti imegoma kutoka ndani mpaka uondoke",aliondoka kwa aibu mno.

3.Nasari alijawa na kiburi na dharau. Kwa mtu yoyote aliyeajiriwa,ukiomba ruhusa huondoki eneo la kazi bila kuhakikisha umeruhusiwa,vinginevyo utakua umejiruhusu.

Eneo lingine aililokosea Nasari,ni kudhani kuna huruma kwenye sheria,Ndugai anaweza kuwa na huruma,ila siyo sheria anazozisimamia. Nimesoma posts nyingi na comments nyingi humu JF,wengi wanamtukana Ndugai na kusahau kuwa siyo yeye,ni sheria.

Wanasema za mwizi ni 40,jitahidi kuhesabu,zikifika 38 tulia kidogo,kwamaana Nasari alipaswa kuwa anaenda bungeni japo mara mojamoja.

Alipokosea tena ni kubase tatizo lake na tatizo la mkewe,alokua anajifungua na mke,siyo yeye,ana dada zake,ana mama yake,mke ana ndugu zake wa kike,walitosha sana kuwa watu wa karibu mke wake,yeye alitakiwa awe kuhenya kutafuta nguo za mtoto na chakula cha mzazi.

Lingine ni kulia mbele za kamera. Mwanaume halii hata sikumoja chozi likaonekana,labda msibani,nako kuna watu wa kukuambia"vumilia,jikaze,wewe ni mwanaume". Huambiwi haya kwa bahati mbaya,ni kukumbusha kuwa,uwe na ngozi ngumu. Unaanguka,unasimama tena.

Mwisho,sioni logic ya yeye kwenda mahakamani. Kufanya nini?,kumshtaki nani?,ili iweje?,katiba inasemaje?,ana barua ipi iliyomruhusu kutokuhudhuria vikao?,anataka kumfurahisha nani kuwa ameenda kuitafuta haki ila imeshindikana?

Yote haya,jibu lake ni kujisumbua,bunge ni muhimili mwingine,mahakama na serikali ni muhimili mwingine.

Pia,asome tu alama za nyakati.

Post a Comment

 
Top