Nabella Banji Kunyolewa Kwapa na Producer Daxo Chali
Baada ya stori nyingi kusambaa kuwa muandaaji wa muziki kutoka katika studio ya MJ Record Daxo Chali, anajihusisha kimapenzi na wasanii wake wa kike hili limeanza kujidhihirisha baada ya Meneja huyo kupost picha inayomuonyesha akimnyoa nywele za kwapa msanii wake mpya Nabella.
Nabella ambaye ni msanii mpya kwa Daxo Chali baada ya Haitham na Nini kuondoka kwa meneja huyo na kulalamika kwamba meneja huyo aliwataka kimapenzi, Nabella amesema yeye hajaona tatizo lolote kufanya kazi na Daxo na katika maisha yake ya muziki asilimia 80 anapata msaada kutoka kwa Daxo Chali.
Nabella akizungumza na eNewz amesema kuwa "Nilikuwa free kunyolewa na Daxo Chali, kwakuwa ndiyo meneja wangu na ndo mtu pekee ambaye nilikuwa nimemzoea kwenye eneo ambalo tulikuwepo tukifanya video ya wimbo wangu Tukumbushie ambao ni wimbo wangu wa pili kutoa hivyo naomba sapoti ya mashabiki zangu kwa hali na mali".
Hata hivyo Nabella alimalizia kwa kuwataka radhi mashabiki zake kuhusu picha iliyosambaa mitandaoni na kusema kwamba picha hiyo ni ajali kazini na ilibidi hali ile itokee kwa kuwa tayari walikuwa nje ya muda na alikuwa akitaka kuwa free kwenye video yake hiyo kujiachia na kuruka sana ndo maana akaona ni vyema kupunguza nywele za kwapa kwa kuwa yeye ni mtoto wa kike usafi ni muhimu kwake.
Post a Comment