Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kilichofanywa na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ni dhambi ya usaliti na haitamwacha salama.
Utakumbuka hapo jana Marchi 18, 2018 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif alitangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Hiyo ni baada ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kumtimua kiongozi hiyo
"Haruna umeamua kuibomoa CUF, Mungu atakulaani wewe na washirika, umeamua kuuvua utu wako kwa mshiko? Ni wazi kazi umeimaliza najua 2020 utarudi kwa waliokutuma, dhambi ya usaliti itakutafuna wewe na kizazi chako," amesema Lissu.
Pia hapo jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilikubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini wa kumtambua Prof. lbrahimu Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi CUF, huku ikitupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na Maalimu Seif aliyeomba mahakama kutoa amri ya kubatilisha barua ya Msaji|i wa Vyama ya kumtambua Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment