KAZI ipo! Mwanamitindo ambaye jina lake limezidi kupaa kutokana na umbo lake tata, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amesema kuwa mwanaume ambaye atampenda na kumuoa lazima ajipange kisawasawa.
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Sanchi alisema kazi yake ya unamitindo imemfanya kupata dili kubwa kwenye kampuni ya nguo za ndani ya Sedative hivyo ataendelea kupiga picha zinazoacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake, kwa hiyo mwanaume huyo ajiandae kwa changamoto hiyo.
“Sidhani kama nikiolewa nitaacha kupiga picha za aina hiyo kwa sababu ni kwa ajili biashara hivyo kama ni mume, inabidi anivumilie na ajifanye kufumba macho,” alisema Sanchi ambaye kila kukicha anaachia picha tata za kuacha watu midomo wazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment