Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike ameongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Tanzania wa mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Uganda unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam siku ya Jumapili ya March 24 2019.
Taifa Stars ipo nafasi ya pili katika Kundi lao L lenye timu za Uganda, Tanzania, Lesotho na Cape Verde lakini ili Tanzania ifuzu ni lazima ifanikishe ushindi katika mchezo huo ukiachilia mbali Uganda wao tayari wamefuzu wanacheza kukamilisha ratiba tu kwani ndio vinara wa Kundi.
Amunike ameeleza na kuwatia moyo watanzania kuwa inawezekana kama waliondoka na point moja Kampala kukiwa hakuna mtu aliyekuwa anatarajia, tutashindwaje tukiwa nyumbani Tanzania katika uwanja wetu, mashabiki wetu na familia zetu.
“Sio mchezo wa kuhusu kushambulia tu unatakiwa kubalansi kushambulia na kujihami pia huu ni mchezo wa mpira wa miguu, unatakiwa ujue namna ya kucheza ukiwa na mpira na ujue kucheza ukiwa hauna mpira, unaangalia mwenyewe namna utakavyo umudu mchezo, unaweza kushambulia ikakusaidia pia”>>>Emmanuel Amunike
“Ni kweli Uganda ni wazi na ukweli pia Tanzania ni wazuri pia, tuliweza kwenda Kampala Uganda na tukaondoka na point pale katika kipindi ambacho hakuna aliyetarajia, sasa tunacheza nyumbani mbele ya familia zetu, mbele ya baba zetu mbele ya dada zetu ila tunatakiwa tuamini katika ndoto yetu kama itawezekana tutafuzu AFCON 2019”>>> Amunike
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment