Msanii Haitham ambaye hivi karibuni ameibua mzozo baada ya kudai Amber Lulu amemchukulia mume wake anayejulikana kwa jina la Niite Boshen, ameweka wazi ukweli wa suala hilo, na kumtaja Amber Lulu kama mwanamke asiye na sifa za kuwa mwanamke wake.
Akizungumzia hilo Haitham amesema kwamba alianza kuona viashiria vya wawili hao muda mrefu wakati Amber Lulu akija kuchora tatoo kwa mume wake, lakini alikuwa akishindwa kufuatilia kwa sababu hakuwa na ushahidi.
Haitham ameendelea kuelezea kwamba hakuna asiyejua kuwa Amber Lulu hawezi kutulia na mwanaume mpaka kufikia hatua ya kuchukua mwanaume wake, ambaye alikuwa akimchora tatto za bure.
Asimulia kwa hasira
“Amber ana tamaa, hawezi kuridhika na mwanaume mmoja, wote tunafahamu, akaona sasa yule alikuwa anamchora tattoo za bure, isiishie hapo tu akachore na mengine, ila mimi nilianza kuona viashiria vyao tu sivielewielewi sema nikawa sifuatilii. Juzi nilikuwa home na mtoto, from no hwere napigiwa simu oya unajua mume wako yuko sehemu fulani, wakati jana yake alinipigia simu mimi nasafiri, kumbe aliniektia akaondoka na yule”, amesema Hitham kwa hasira.
“Who is Amber Lulu, ni mwanamke gani, ukimuangalia ukinilinganisha na mimi huwezi kutulinganisha, akaona mimi kuwa na Bosheni kama nafaidi, mimi hainipi stress”, ameendelea kusema Haitham.
Kwa upande wa Amber Lulu ameonekana kutojali linaloendelea huku akiendelea kumpost mwanaume huyo, na kumuwekea alama za makopa kopa na caption za kumchamba.
Haitham na Niite Boshen wamezaa mtoto mmoja wa kike, na imeelezwa kuwa wawili hao walifunga ndoa rasmi.
Post a Comment