MSANII mrembo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Ester Kiama, amefunguka kuwa kila akimuangalia Mwanamama Zarina Hassan ‘Zari the Bosslady’ akiwa anapata dili za matangazo anaumia sana na wakati mwingine usingizi unakata na kujiuliza yeye anapataje na si Mbongo.
Akichonga na Za Motomoto, Ester alisema kuwa, madili makubwa anayopata Zari, yanatakiwa kuwafanya mastaa Bongo wajifunze na wajiulize maswali mengi kwa nini yeye tu na sisi tupo hatuna hili wala lile?
“Jamani yaani fursa anazopata Zari, kuna wakati mwingine zinanichanganya sana kwa sababu najiuliza mbona sisi hatuwezi inakuaje yeye hapo ndipo nachanganyikiwa mimi, ” alisema Ester.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment