0

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lindi Vijijini, Athuman Seif Mwomonyoko amepokea wanachama kumi na moja kutoka chama cha wananchi CUF kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mnyangara Kata ya Mipingo Jimbo la Mchinga mkoani humo.

Katika mapokezi hayo, Mwomonyoko amewaahidi wanakijiji wa kijiji hicho kuwa nao bega kwa bega katika kuhakikisha uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unakuwa wa usalama, amani na ameahidi kuwashughulikia wale wote ambao wamejipanga kuvuruga uchaguzi huo.

Aidha, Mwenyekiti huyo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule, kwani elimu ndiyo msingi wa maisha lakini pia ndio chanzo cha maendeleo yao ya baadae katika kijiji hicho.

Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Lindi Vijijini, Abdallah Omar Mtambule, amewaomba wanakijiji kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu 2020 kama waliyoyafanya 2015 kwani makosa yao ndiyo yamefanya kijiji hicho kutokuwa na upatikanaji wa huduma za kijamii hususani Maji, Barabara, Umeme na kituo cha afya kwani hayo yametokana na kutowajibika kwa kiongozi ambaye.

Post a Comment

 
Top