0



Clouds Media Group mwaka huu imepata pigo zito baada ya kuondokewa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, ndugu Ruge Mutahaba. Wakiwa bado na machungu ya kuombeleza msiba huo mzito ndani ya kampuni hiyo, waliondokewa tena na mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde ambaye alifariki siku chache baada ya kumzika Ruge.


Bongo5 imekuandalia mambo matano ambayo bado yataendelea kukibeba kituo cha Clouds Media licha ya kuwapoteza watu wake muhimu ambao walikuwa na mchango mkubwa wa kuifanya kampuni hiyo kuwa super brand kwa miaka mitatu mfululizo.

Legacy aliyoiacha Ruge 

Ruge ambaye amekaa Clouds Media kwa zaidi ya miaka 20, amefanya project nyingi ambazo zitamfanya aendelee kukumbukwa daima na kituo hicho na kuendelea kutembea kifua mbele. Kuendelea kufanyika kwa Fursa, Malkia wa Nguvu, pamoja na uwepo wa Fiesta ni vitu ambavyo vitakifanya kituo hicho cha redio na runinga kuendelea kutamba kwa kuwa kinaendelea kugusa maisha ya vijana katika nyanja mbalimbali.

Ruge amewatengeneza watu ambao wanatembea na kivuli chake ndani Clouds

Katika uhai wake Ruge alimchukulia kila mafanyakazi wa Clouds kwake ni wakipekee. Kila mfanyakazi ata-shine kwa uwezo wake na sio kubebwa, alithamini kipaji zaidi kuliko elimu. Kitu hichi kimewafanya wafanyakazi wengi kujiamini na kufanya vitu vyao vya ziada hali ambayo imetengeneza majina yao na kuwa mkubwa nchini Tanzania. Vijana hao bado wataendelea kufanya mazuri kwa kuwa ni wanafunzi wa master na wengi walikulia mikononi kwake.

Wiki hii tumeshuhudia nafasi ya Kibonde kwenye Jahari ilichukuliwa na PJ ambaye alikuwa Power Breakfast Clouds Fm, na Samsasali wa Clouds 360 akiziba nafasi ya PJ ndani ya PB. Mageuzi yote huwenda yakawa na tija, kama nilivyoeleza awali kwamba Clouds tayari ina mtaji wa watu, ina vinaja wengi wa ndani na nje ambao wamewaandaa kwa muda mrefu.

Maudhui

Kama unavyojua media zinahitaji maudhui bora ili iweze lufanya vizuri. Wananchi wanahitaji kuguswa maisha yao ili waweze kukufuatilia, Media House ikiachana na kutoka habari, kuelimisha na kutoa burudani lakini kuna mambo mapya kwa sasa yameongezeka, kutoa fursa, kutafuta majibu ya changamoto zao, pamoja na kuwaonganisha watu na kugusa maisha ya watu wa chini kupitia matukio mbalimbali. Clouds wamekuwa kinara kwenye hilo, ukiangia matukio kama Nguvu ya Binti, Fursa na Fiesta ni moja kati ya project ambazo zitaendelea kugusa maisha ya watu moja kwa moja

Tasnia ya Muziki.

Clouds toka siku ya kwanza walianza kuupa thamani zaidi muziki wa BongoFleva kuliko muziki mwingine, waliamua kuwa-selective katika aina ya muziki wanaoufanya huwenda ndio kitu pekee kimewafikisha hapo walipo sasa. Kwa mantiki hiyo bado wataendelea kuangaliwa kwa jicho la tofauti, bado mashabiki wataendelea kusikiliza muziki nzuri kwa kuwa tayari wana misingi ambayo wamekuwa wakiishi nayo katika nyanja hizo.

Mahusiano ya Redio na watu wa nje (The People Station)

Redio ikiweza kugusa maisha ya watu moja kwa moja lazima itakuwa chaguo la namba moja, kwanini mtu aache kusikiliza redio ambayo inampa habari kwa style ya kileo, inam-burudisha na kumpatia deals na network za kibiashara. Clouds toka siku ya kwanza wanalia na vijana ndio maana kikazaliwa kitu kama Fursa, Maklia wa Nguvu.

Yote hayo nikutengeneza mahusiano ya moja kwa moja na mashabiki wao ambao wakipata habari wanataka pia kujua wapi wataenda kuuza bidhaa zao.

Rais Magufuli aliwahi kupiga simu Clouds akionyeshwa kufurahishwa na namna wanavyoendesha vipindi vyao, kama Rais aliwakubali nani atawakataa bado wana nafasi kubwa. Kila la heri Clouds.

Bongo5

Post a Comment

 
Top