CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswallo Mganga kuchunguza kesi ya mauaji kwa madai kuwa watuhumiwa walibambikiziwa kesi huku kikiiomba serikali kupitia DPP huyo kuunda tume maalum itakayochunguza kesi mbalimbali za makosa ya jinai nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho leo Jumatano, Machi 20, 2019, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amesema watuhumiwa wengi waliopo mahabusu kesi zao huchukua muda mrefu kupepelezwa na wengine hubabimbikiziwa kesi jambo ambalo halikubaliki.
Mwalimu amesema hayo baada ya DPP Biswalo, kuawafutia shitaka la mauaji watuhumiwa Musa Sadiki na Edward Matiku kufuatia agizo la Rais Magufuli la kuchunguzwa kwa kesi hiyo baada ya kusoma katika gazeti moja ambapo Musa Sadiki aliandika barua ikionesha alivyobambikiwa kesi ya mauaji na jeshila polisi huku wakichukua fedha taslim Tsh. 788,000 na simu ya mkononi.
Aidha, DPP aliagiza polisi kuwachunguza waliohusika katika kupanga kesi hiyo namba 8/2018 mkoani Tabora ili wachukuliwe hatua huku akiweka sharti la kutaka kesi zote za jinai zipitie ofisi yake kabla ya kwenda mahakamani.
Aidha, Mwalimu amesema vyombo vya usalama nchini vina wajibu mkubwa wa kuhakikisha utu wa mtu haupotei na kama watamtia hatiani mwananchi basi upelelezi ufanyike kwa haraka badala ya kuendelea kusota rumande.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment